Prokulo, Eutisi na Akusi

Kifodini cha Mt. Januari kadiri ya Artemisia Gentileschi (1636). Shemasi Prokulo anaonekana chini kushoto.

Prokulo, Eutisi na Akusi (walifariki Pozzuoli, mkoa wa Campania, leo nchini Italia, 19 Septemba 305) walikuwa Wakristo wa mji huo waliouawa kwa ajili ya imani yao pamoja na askofu Januari na wengine watatu wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1][2].

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa hasa tarehe 18 Oktoba[3].

  1. J. Stilting (1703-1762), Acta ss. Januari episcopi, Sosii, Festi et Proculi diaconorum, Desiderii lectoris, Eutychis vel Eutychetis et Acutii martyrum Puteolis in Campania felice, commentario e notationibus illustrata a Joanne Stiltingo, Antuerpiae, apud Bernardum Albert Vander Plassche, 1757.
  2. Santi Procolo, Eutiche e Acuzio
  3. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search